Kilimo Ajira - Kilimo cha mimea na miti
Tunaangazia kilimo cha mimea na miti kwa mseto. Hivi unajua miti ni mojawapo ya nguzo ambayo ni muhimu zaidi katika kilimo cha mimea? Kwa mujibu wa takwimu za shirika la utafiti wa misitu nchini KEFRI, Kenya ina asilimia 7 ya miti inayotengeneza misitu ya kienyeji sawia na hekari milioni 200 huku hekari milioni 15 ikiwa ni misitu inayotokana na juhudi za watu kupanda.
Misitu na miti huchangia kuimarisha kilimo kwa kuhakikisha hali nzuri ya anga ambayo husababisha kuwepo kwa mvua. Kadhalika, miti husaidia pakubwa kuimarisha na kuulinda udongo.