Kilimo Ajira - Mbolea
Tunaangazia mbinu ya kutengeneza mbolea asili isiyo na kemikali. Mazao katika mashamba mengi meaneo mbalimbali humu nchini yanazidi kupungua ,kutokana na hali ya udongo kukosa rotuba. Kiini kamili cha ukosefu wa rotuba ni matumizi ya mbolea za kisasa zilizo na kemikali na ambazo husababisha mchanga kuwa na asidi nyingi.
Safari ya kukutana na wakulima walioekeza katika kutengeneza mbolea ya kiasili inatufikisha Ugunja kaunti ya Siaya.