Kilimo AJira – Ufugaji wa kuku wa kienyeji

Kilimo AJira - Ufugaji wa kuku wa kienyeji

Tunaangazia mbinu za ufugaji wa kuku wa kienyeji hasa manufaa ya ufugaji wa kuku wa kienyeji walio na nyama yenye ladha, idadi kubwa ya mayai na mauzo ya kuku hawa wenye afya. Sawia na nchi zingine barani Afrika, kilimo cha kuku kimekumbatiwa zaidi na akina mama katika jamii za humu nchini. Kikawaida kuku hutolewa nje nyakati za asubuhi na kuruhusiwa kurejea vibandani wakati wowote wa siku.

Familia nyingi maeneo ya magharibi mwa Kenya hufuga kuku wa kienyeji huku ikibainika kwamba kuku chanzo muhimu cha protini na pia huleta mapato ya ziada kwa wafugaji. Baadhi ya akina mama wakulima wa kuku Kakamega wanatuelezea namna wanavyoendelea kufaidika kutukona na ufugaji wa kuku wa kienyeji na njia rahisi ambazo zinawasaidia kuwa na kuku walio na afya nzuri